Akizungumzia matukio ya hivi majuzi kati ya India na Pakistan, Araghchi amesema: "India na Pakistan ni nchi mbili ndugu na majirani wa Iran, na zina uhusiano uliokita mizizi katika mafungamano ya kitamaduni na ustaarabu ulioanzia karne nyingi zilizopita."
"Tunawazingatia, kama majirani wengine, kuwa ni kipaumbele chetu cha kwanza", amesisitiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.
Sayyid Araqchi ameongea kuwa: "Tehran iko tayari kufanya juhudi za upatanishi kati ya Islamabad na New Delhi ili kukuza maelewano kati ya pande hizo mbili katika nyakati hizi ngumu. Huu ndiyo moyo tuliofundishwa na mshairi wa Kiajemi Saadi: "Wanadamu ni viungo vya mwili mmoja. Wameumbwa kutokana na kito kimoja, na
kama kiungo kimoja kitapata maumivu, viungo vingine vyote pia huhisi maumivu."
Mzozo wa sasa kati ya New Delhi na Islamabad umeibuka baada ya watu waliokuwa na silaha kulifyatulia risasi kundi la watalii katika eneo la kitalii la Pahalgam, lililoko takriban kilomita 90 kutoka Srinagar, mji mkuu wa majira ya joto wa Kashmir inayodhibitiwa na India, na kuua watu wasiopungua 27, Jumanne ilioyopita.
Maafisa wa serikali ya India wamelitaja tukio hilo kuwa ni shambulizi la kigaidi. India inamtuhumu jirani yake wa magharibi (Pakistani) kuwa imehusika katika shambulio dhidi ya watalii huko Kashmir.
Hata hivyo, Seneta Muhammad Ishaq Dar, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, amelitaja tukio hilo kuwa ni la kusikitisha na wakati huo huo ameonya dhidi ya vitendo vyovyote vya uchochezi vinavyofanywa na jirani yake wa mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan amesema: "Kama nguvu ya nyuklia, Islamabad italipiza kisasi dhidi ya hatua yoyote ya India ili kulinda maslahi yake ya kitaifa."
342/
Your Comment